Monday, 23 October 2017

STATOIL YASISITIZA UJENZI WA MTAMBO WA KUSINDIKA GESI


KAMPUNI ya utafiti na uchimbaji wa gesi ya Statoil ya Norway imesema serikali inapaswa kuona kipaumbele cha kufikia makubaliano ya kujengwa kwa mtambo wa kusindika gesi ya kimiminika (Liquified Natural Gas – LNG) kwa faida ya usafirishaji wa gesi hiyo kwenye soko la kimataifa pamoja na matumizi ya ndani.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na kampuni yake, Meneja Mkazi wa Statoil, Øystein Michelsen, alisema mtambo wa LNG ndio utakaosaidia kuchakata na kusindika gesi hiyo ili kurahisisha kuisafirisha nje.

“Huwezi kusafirisha gesi katika hali yake ya kawaida, ni lazima kuisindika kwa kuibadili kuwa katika hali ya kimiminika, hivyo mtambo wa LNG una umuhimu mkubwa kwa biashara ya gesi kwa kusafirisha kwenye soko la kimataifa pamoja na matumizi ya ndani,” alisema Michelsen.

Statoil na mshirika wake ExxonMobil wamefanya ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika visima vya Zafarani, Lavani, Tangawizi, Piri, Giligilani na Mronge katika Kitalu namba 2, chenye eneo la takriban kilometa za mraba 5,500, ambalo lipo umbali wa zaidi ya kilometa 100 kutoka ufukweni katika kina cha maji kati ya meta 1,500 hadi 3,000.

Na Daniel MbegaReactions:

0 comments:

Post a Comment