Monday, 30 October 2017

MWANAFUNZI ALIWA NA MAMBA MOROGORO

Image result for crocodile

MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Mwaya iliyopo Wilayani Ulanga mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kuvamiwa na mamba wakati akioga pamoja na wanafunzi wenzake mtoni.

Diwani wa kata ya Mwaya na diwani wa Kata ya Chirombolo wamesema matukio hayo yamekithiri zaidi katika kata hizo mbili hali inayopelekea wakazi wa kata hizo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kuhofia kuvamiwa na mamba na kulazimisha wakazi wengi kulala mapema.


Kwa upande wao viongozi wa Wilaya ya Ulanga wakiwemo madiwani wa halmashauri hiyo, wanasema wameandaa mpango mkakati wa kuweza kudhibiti kero hiyo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment