Thursday, 5 October 2017

MLIMA KILIMANJARO WAINGIA TUZO ZA VIVUTIO BORA VYA UTALII DUNIANI


Tanzania na Mlima Kilimanjaro imeorodheshwa kwenye tuzo za vivutio bora vya utalii zinazotarajiwa kutolewa Desemba, mwaka huu.

Tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirika la World Travel (WTO) ambazo zinatolewa kwa mara ya 24 mwaka huu, zimeiweka Tanzania kwenye kipengele cha nchi bora kuzitembelea kutokana na vivutio ilivyonavyo, wakati Mlima Kilimanjaro ukishindania kivutio bora cha utalii duniani.

Tuzo hizo zitakazotolewa kutokana na wingi wa kura ambazo kila kivutio kitapata kutoka kwa watalii, wataalamu wa sekta hiyo na watoa huduma, zitahitimishwa Desemba 10 nchini Vietnam.

Kwenye kipengele cha nchi yenye vivutio vingi, Tanzania inachuana na Botswana, Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Mlima Kilimanjaro unachuana na vivutio vingine vya jengo refu la Burj Khalifa (Dubai), Ferrari World (Abu Dhabi), The Great Wall (China) na Intramuros (Ufilipino).

Vivutio vingine vilivyo pamoja na mlima huo mrefu zaidi Afrika ni Las Vegas Strip (Nevada, Marekani), Machu Picchu (Peru), Spike Island (Ireland) na Mlima Sugarloaf.


Kupata ushindi, wadau wanatakiwa kujiandikisha na kupiga kura za kutosha kupitia tovuti ya waandaaji ambayo ni www.worldtravelawards.com/register

Reactions:

0 comments:

Post a Comment