Thursday, 12 October 2017

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI DAR

Image result for wauwa kwa risasi

WATU wawili wanaohisiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi, mmoja akituhumiwa kuhusika katika tukio la kuvamijiwa na kujeruhiwa Meja Janerali Mstaafu, Vicent Mritaba.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano saa nne usiku eneo la Mbezi Mshikamano kwa Mgalula.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Kamanda Mambosasa amesema mtuhumiwa anayehusishwa na kumjeruhiwa Meja Jenerali mstaafu Mritaba pia aliwahi kufungwa.

"Ametumikia adhabu ya kifungo mara kadhaa na alipotoka aliendelea na shughuli zake na jana ndiyo ilikuwa mwisho wake," amesema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment