Thursday, 5 October 2017

HUKUMU KESI YA MANJI KUTOLEWA KESHO

Image result for YUSUPH MANJI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesho inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji (41).

Hukumu inatarajia kutolewa kesho Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.

Katika kesi hiyo, upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi saba na wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watatu. Awali, Manji kupitia wakili wake Hajra Mungula aliieleza Mahakama kwamba angekuwa na mashahidi 15.

Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Ushahidi wa upande wa utetezi mahakamani unaonyesha Manji ana vyuma kwenye moyo. Mfanyabiashara huyo katika utetezi wake alidai ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka kwa babu zake na alianza kuugua akiwa na miaka 26.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment