Tuesday, 3 October 2017

CHAMA CHA UPINZANI CHATANGAZA KUFANYIA MKUTANO MKUU IKULU DAR


Chama cha Upinzani cha CCK hapa nchini kimesema kinajiandaa kufanya mkutano wake mkuu katika ukumbi wa Ikulu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli, siku chache baada ya rais Magufuli kusema kuwa ukumbi huo ni wa Watanzania wote.

Mwenyekiti wa CCK Bw.Contastine Akitanda amesema baada ya Rais Magufuli kusema kuwa ukumbi huo ni watanzania chama chake kitaitekeleza kauli hiyo kwa kufanya mkutano wake mkuu mapema mwakani 2018.

Ameongeza kuwa walitaka kuomba ukumbi huo wa Ikulu kwa ajili Kikao cha Kamati Kuu wiki ijayo lakini wameona kikao hicho kitakua na wajumbe wachache takribani 30, sasa wanajiandaa kufanya mkutano mkuu utakaokuwa na wajumbe 500 kwa kuwa ukumbi ule ni mkubwa.

Hivi karibuni chama cha Chadema kimeilalamikia Serikali ya Rais Magufuli kukiuka sheria ya Vyama vya siasa inayokataza vyama vya siasa kutumia rasilimali za serikali kwa manufaa ya chama cha Mapinduzi (CCM).


Chama Cha Kijaamii cha CCK ni zao la chama (CCJ) kilichofutwa rasmi 23.7.2010

Reactions:

0 comments:

Post a Comment