Wednesday, 11 October 2017

CHADEMA WAKATAA KUZIBWA MIDOMO

Image result for SALUM MWALIMU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kikiwa kama chama kikuu cha upinzani kitaendelea kuikosoa na kuishauri Serikali kwakuwa ni wajibu wao kuwazungumzia wananchi.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu amesema hayo leo na kudai kuwa hivi karibuni kumekuwepo juhudi nyingi za makusudi za kuwaziba midomo.

Amesema hawatakubali mitutu wala nini, kwakuwa wamezaliwa siku moja na watakufa siku moja.

“Tutasema, tutakosoa na kukemea na hatutakubali kurudi nyuma hata siku moja na tunawahakikishia Watanzania hatutarudi nyuma,” amesema.

Amesema mwaka jana walijaribu kuzungumzia mambo hayo kupitia operesheni Ukuta, ili kueleza kile walichokiona ambacho kingekuja siku za usoni na sasa ndicho kinachotokea.

“Wako waliodhani matukio haya yataturudisha nyuma, hakuna jambo jema kama mshindani wako anapokuwa hoi na kweli wako hoi,” amesema Mwalimu.


“Tuliwaambia Watanzania harufu hii ya kutokuheshimu Katiba, Sheria na ilianza kwa kuzuia mikutano, kamata weka ndani saa 48 wakasema si wanasiasa na tukawaambia ukiukwaji huu wa kisheria hautaishia kwa wanasiasa na ndicho kinaonekana kutokea sasa,” ameongeza Mwalimu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment