Wednesday, 11 October 2017

BAADA YA ODINGA KUJITOA, DK AUKOT ARUHUSIWA KUWANIA URAIS KENYA

Image result for EKURU AUKOT

Wakati aliyekuwa Mgombea Urais nchini Kenya kwa tiketi ya NASA, Raila Odinga, akitangaza hapo jana kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa marudio, Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru mgombea urais wa chama cha Thirdway Alliance, Dkt. Ekuru Aukot, aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu wa awali wa Agosti 8, ashirikishwe kwenye uchaguzi wa marudio unaopangiwa kufanyika tarehe Oktoba 26, mwaka huu.

Awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka Kenya, IEBC ilikuwa imetangaza kwamba ni wagombea wawili pekee, Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa Muungano wa National Super Alliance (Nasa) wangechuana katika uchaguzi huo wa marudio.Reactions:

0 comments:

Post a Comment