Saturday, 30 September 2017

PROFESA MAGHEMBE AZINDUA MAONESHO YA UTALII YA KARIBU KUSINI, MJINI IRINGAWaziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe jana amezindua maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa.

Maonesho hayo yanayokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya utalii duniani yanalenga kutangaza vivutio vya utalii vya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na shughuli za wajasiriamali kutoka pembe mbalimbali za nchi.

Pamoja na kuzindua maonesho hayo yanayofanyika hadi Oktoba 2 katika viwanja hivyo, Prof Maghembe alizindua mpango mkakati wa utalii wa mkoa wa Iringa pamoja na Jarida la Utalii la mkoa huo.

Akizindua maonesho hayo alisema kwa kupitia Mpango Kabembe (Master Plan) ya wizara, serikali itauendeleza mkoa wa Iringa ili ile azma ya kuufanya mkoa huo kuwa Kitovu cha Utalii Kusini ilete tija.

Katika maonesho hayo ambayo kauli mbiu yake ni Utalii Endelevu ni Nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika wadau zaidi ya 350 kutoka mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Katavi na Rukwa inayounda kanda hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema maonesho hayo yataendelea kufanyika kila mwaka mjini Iringa kwa lengo la kuutangaza vivutio vya utalii kusini, kufungua fursa mbalimbali na kuinua uchumi wa wakazi wa mikoa ya kanda hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment