Tuesday, 26 September 2017

NDUGU SITA KUNYONGWA HADI KUFA

Image result for MAHAKAMA KUNYONGA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewahukumu adhabu ya kifo watu sita ambao ni ndugu wakazi wa Kalambo baada ya kupatikana hatia ya kumuua ndugu yao.

Ndugu hao wamedaiwa kwamba walifikia uamuzi wa kumuua ndugu yao huyo kwa madai ya kwamba anajihusisha vitendo vya kishirikiana.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne na Jaji Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliopeleka mashahidi sita ili kuthibitisha mashitaka hayo.


Waliokutwa na hatia katika shauri hilo ni Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo, Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick Nguvumali na Anatory Kamande huku Alistid Kamande na Will broad Kamande wakiachiwa huru kwa kutokutwa na hatia.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment