Thursday, 7 September 2017

MTUHUMIWA WA UTEKAJI WATOTO AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI

Image result for Kijana mtekaji watoto, Samson PetroKIJANA wa miaka 18 aliyekuwa anatuhumiwa kuhusika na matukio ya utekaji watoto akitaka wazazi watoe fedha ili kuwaachia watoto hao, Samson Petro amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Jeshi la Polisi.

Kijana huyo anadaiwa kupigwa risasi alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi na kufariki dunia katika Hospitali ya Mount Meru, Jijini Arusha.

Kabla ya kukamatwa, kijana huyo anadaiwa kusababisha vifo vya watoto wawili, Maureen David na Ikram Salim ambao aliwadumbukiza katika shimo la choo kilichokuwa hakitumiki baada ya kukosa fedha kutoka kwa wazazi wao.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment