Sunday, 24 September 2017

LEMA, NASARI WAZUNGUMZIA JINSI RUSHWA INAVYOWAHAMISHA MADIWANI WAO

Image result for lEMA NASARI

Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari wanatarajia kuanika siri ya madiwani kumi wa Chadema kuhamia CCM na kupokelewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Kupitia ujumbe wa Video uliowekwa na viongozi hao mtandaoni, Godbless Lema wa Arusha Mjini pamoja na Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki wamemtaka Rais Magufuli kuwapatia nafasi za kuweza kumthibitishia jinsi viongozi wake walivyoweza kutumia rushwa na kuwashawishi madiwani hao wa Chadema kuachia ngazi.

Aidha, Joshua Nassari amesema leo watafanya mkutano na wanahabari na kuelezea rushwa ilivyotumika na viongozi kumdanganya Rais wa nchi na kusisitiza ushahidi wao hauna mashaka.


Baada ya Rais Magufuli kuhutubia Arusha katika shughuli za kuwatunukia Kamisheni Maafisa ya Jeshi la Wananchi JWTZ jana amewapokea Madiwani kumi waliohama Chadema kwa madai ya kumuunga Rais mkono.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment