Monday, 25 September 2017

AJALI YA BASI YAUA NA KUJERUHI MKOANI SHINYANGA


MTU mmoja aliyetajwa kwa jina la Lucas Maganga (25) mkazi wa Shinyanga mjini amefariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la Allys lenye namba za usajili T 979 CDH lililokuwa linatoka Ushirombo kwenda Bariadi mkoani Simiyu.

Ajali hiyo imetokea mapema leo katika eneo la Maganzo mkoani Shinyanga baada ya basi  kupasuka gurudumu la mbele. Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment