Tuesday, 1 August 2017

WEMA ASHINDWA KUPOKEA RASMI KADI YAKE YA CHADEMA LEO

Image result for wema sepetu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye, ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi rasmi kadi ya chama hicho aliyekuwa mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.

Tukio hilo lilipangwa kuhitimisha tangazo la wema miezi kadhaa iliyopita kujiondoa Chama cha Mapinduzi(CCM) na akijiunga na Chadema.

Akizungumza na waandishi leo wakati akitangaza kuahirisha mkutano huo, Sumaye, ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu katika awamu ya Tatu, alisena tukio hilo limeahirishwa kwa sababu Wema ameshindwa kufika kutokana na kubanwa na ratiba za Mahakama.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment