Tuesday, 29 August 2017

MBUNGE WA TUNDUMA AKAMATWA NA POLISI

Image result for MBUNGE WA TUNDUMA

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Mhe.Frank Mwakajoka (CHADEMA) kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais.

Wateule hao ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa Songwe, Chiku Galawa na Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando.


Mbunge huyo tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi. Bado haijafahamika dhihaka hiyo iliyotolewa na mbunge huyo ni ipi, hivyo mpendwa msomaji endelea kuwa nasi kwa habari zaidi juu ya sakata hili.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment