Wednesday, 9 August 2017

KURA ZA URAIS ZABUBUJIKA KWA UHURU KENYATTA, ODINGA APINGA

Image result for kenya election results

ASILIMIA 92 ya kura zilizopigwa katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika jana Jumanne zimekwisha hesabiwa, huku Rais Uhuru Kenyatta akimuacha kwa mbali mpinzani wake mkuu wa Muungano wa Upinzania (Nasa), Raila Odinga.

Matokeo yaliyotangazwa saa nne asubuhi ya Jumatano ya leo, yanaonesha Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee alikuwa akiongoza akiwa na kura 7,656,951 sawa na asilimia 54.5 akifuatwa na Raila Odinga wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) alikuwa na kura 6,274,821 sawa na asilimia 44.7.

Muungano wa Nasa umepinga matokeo yanayoendelea kutangazwa na tume hiyo na kusema si sahihi.

Odinga amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imefanya makosa kutangaza matokeo hayo bila kuwaonyesha mawakala wa vyama Fomu 34A, kubainisha matokeo hayo yametoka katika vituo gani.

Ili kushinda, mgombea urais anahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa, na angalau asilimia 25 katika kaunti 24 kati ya kaunti 47 nchini humo.

Iwapo hakuna mgombea atakayetimiza hilo, basi uchaguzi wa marudio utafanyika katika kipindi cha siku 30.

Kujitokeza mapema
Wapiga kura walianza kujitokeza alfajiri na mapema kupiga kura.

Foleni ndefu zilishuhudiwa katika vituo vingi, na kwingine visa vya watu kuumia katika mkurupuko wa kupanga foleni vituo vilipofunguliwa viliripotiwa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment