Wednesday, 9 August 2017

KOREA KASKAZINI YAJIPANGA KUKABILIANA NA MAREKANI

Image result for north korean leader military picture

Korea Kaskazini imedokeza kwamba inatafakari uwezekano wa kurusha makombora karibu na Jimbo la Marekani la Guam katika bahari ya Pasifiki, saa chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuitishia Pyongyang kwamba itakabiliwa kwa moto na ghadhabu.

Shirika la Habari la Serikali ya Korea Kaskazini limesema taifa hilo linatafakari mpango wa kurusha makombora ya masafa ya kati na mbali karibu na Guam, eneo ambalo Marekani huwa na ndege zake za kuangusha mabomu.

Taarifa hiyo inaashiria kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili huku Umoja wa Mataifa (UN) ukiidhinisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo hivi karibuni.

Rais Trump ametoa tamko lake baada ya ripoti kwenye vyombo vya habari kusema kwamba Korea Kaskazini imeweza kuunda kichwa cha silaha za nyuklia chenye uwezo wa kutosha kwenye makombora yake.

Ufanisi huo, ingawa haujathibitishwa rasmi, ulitazamwa na wengi kama kiunzi cha mwisho kilichoizuia Korea Kaskazini kuwa taifa kamili lenye nguvu za silaha za nyuklia.


Taarifa ya gazeti la Washington Post, ikinukuu maafisa wa ujasusi wa Marekani, imedokeza kwamba Korea Kaskazini inaunda silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kasi zaidi ya ile iliyotarajiwa. Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema jeshi la nchi hiyo linachunguza kwa makini mpango wa kuanzisha moto wa kuzingira Guam kwa kutumia makombora ya roketi ya masafa ya wastani na ya masafa marefu ya Hwasong-12.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment