Thursday, 31 August 2017

IPTL YANYIMWA LESENI

Image result for mitambo ya IPTL

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imekataa maombi ya kuiongezea muda wa leseni kwa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, baada ya muda wake kumalizika.

Kwa mujibu wa tangazo la Ewura, lililotolewa kama taarifa kwa vyombo vya habari, maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura kilichofanyika Agosti 30, mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine, uamuzi huo umechangiwa na uwepo wa kesi zinazoendelea mahakamani kuhusu umiliki wa Kampuni hiyo baada ya kuuziana hisa huku waliokuwa wabia katika IPTL, Harbinder Singh wa Kampuni ya PAP na James Rugemarila wa VIP Engineering Limited wakiwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kuakatisha fedha.


 “Bodi ya Wakurugenzi ya Ewura katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Agosti 2017, imefikia uamuzi wa kukataa maombi ya kampuni ya IPTL baada ya kuzingatia mambo kadhaa,” ilieleza taarifa hiyo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment