Thursday, 31 August 2017

DK MAKONGORO MAHANGA AINGIA MATATANI

Image result for makongoro mahanga

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga amekamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu.

Inadaiwa kuwa Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.

Kiasi hicho cha fedha ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.


Katika kitabu hicho amemtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi. Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment