Thursday, 10 August 2017

DADI IGOGO ARITHI MIKOBA YA JOSEPH LYATA UNAIBU MEYA MANISPAA YA IRINGA


BARAZA Maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, leo limemchagua Diwani wa Kata ya Gangilonga, Dadi Igogo (Chadema) kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Igogo aliyekosa mpinzani baada ya diwani wa kata ya Nduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Bashiri Mtove kujitoa katika kinyang’anyiro hicho alishinda kwa kupata kura 15 na kunyimwa kura 11 kati ya kura 26 zilizopigwa.

Kwa ushindi huo, Igogo anavaa viatu vya Diwani wa Kata ya Kwakilosa, Joseph Lyata (Chadema) aliyekuwa Naibu Meya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaundwa na madiwani 28 kati yao Chadema ina madiwani 21 (14 wa kuchaguliwa, watano wa viti maalumu na wabunge wawili-Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa Mjini na Suzan Mgonakulima mbunge wa viti maalumu).


Na CCM ina madiwani saba ( wanne wakuchaguliwa, viti mmoja na wabunge wawili wa viti maalumu Rita Kabati na Zainabu Mwamwindi) 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment