Sunday, 13 August 2017

BOMOA BOMOA INAVYOWALIZA WAKAZI WA MOROGORO ROAD

Image result for bomoa bomoa morogoro road

Wakati wakiwa kwenye tafakuri ya wapi pa kwenda baada ya makazi yao kuwekewa alama ya X, wakazi wa Kimara, Mbezi na Kiluvya wanaoishi kandokando ya Barabara ya Morogoro wiki iliyopita walikumbwa na janga jingine la kukatiwa huduma muhimu za umeme na maji ili kupisha ubomoaji wa nyumba hizo.

Chini ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Serikali ina mpango wa kuipanua barabara hiyo kuanzia Kimara hadi Kiluvya, hivyo nyumba zilizopo ndani mita 121.5 kila upande, zinatakiwa kubomolewa.


Uwekwaji wa alama ya X katika majengo yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara hiyo ulianza Mei 2 kwa Tanroads kutoa notisi kwa wakazi wa eneo hilo ikiwataka hadi kufikia Juni 8 wawe wamebomoa nyumba zao. Hali hiyo ilipingwa na wakazi wengi, baadhi wakisema zinazopaswa kubomolewa ni zile zilizo ndani ya mita 30 kila upande wakisema ni 60 na kwamba mita 121.5 ni kubwa mno. Kutokana na utata huo, wapo ambao wamefungua kesi mahakamani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment