Tuesday, 1 August 2017

BEI YA MAFUTA YASHUKA

Image result for KITUO CHA MAFUTA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo ya bidhaa za mafuta aina ya petroli kwa Agosti .

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika kesho zimeshuka kwa Sh36 na Sh44 kwa lita ya petrol na dizeli mtawalio.

Taarifa hiyo inasema kwamba tofauti ni katika mafuta ya taa ambapo bei yake imeongezeka kwa Sh24 kwa lita, hali iliyosababishwa na kuongezeka kwa gharama ya usafirishaji wa bidhaa katika mfumo wa Uagizwaji wa Mafuta kwa Pamoja (BPS).

Wastani wa matumizi ya mafuta kwa siku ni lita milioni tano, milioni tatu na 100,000 kwa dizeli, petrol na mafuta ya taa, sawia.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment