Tuesday, 8 August 2017

ABRAMOVICH ATENGANA NA MKEWE

roman abramovich

BILIONEA wa Urusi na mmiliki wa klabu ya Chelsea ya jijini London, Roman Abramovich amemwagana na mkewe aliyeishi naye kwa miaka 10.

Wawili hao, ambao wana watoto wawili, walitangaza kutengana Jumatatu.

Abromovich na mkewe huyo walisema uamuzi wao ni wa kirafiki na kwamba wamekubaliana kwa pamoja kuwalea watoto wao, Aaron Alexander na Leah Lou. Watoto hao walizaliwa Marekani.

Katika tamko lao la pamoja walisema: “Baada ya kuishi kwa pamoja kwa miaka 10, tumefanya uamuzi mgumu wa kutengana, lakini tutaendelea kuwa marafiki wa karibu, wazazi na washirika katika miradi tuliyoianzisha kwa pamoja.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment