Sunday, 13 August 2017

24 WAUAWA ODINGA WAKIPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU KENYA

Image result for VURUGU ZA UCHAGUZI KENYA

Tume ya haki za Binadamnu nchini Kenya imesema kuwa watu 24 wameuawa katika ghasia za upinzani kupinga matokeo nchini Kenya.

Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya, ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na maandamano wenye nia ya kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo “feki” ya uchaguzi mkuu.

Naye mgombea urais wa Nasa Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi mkubwa wa kura.


Katika uchaguzi huo Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290.. ambayo ni asilimia 54 huku mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akipata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment