Tuesday, 4 July 2017

WILAYA TATU ZAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI UVUVI HARAMU BWAWA LA MTERA

Image result for samaki haramu

SAMAKI aina ya perege na kambale ambao ni maarufu katika Bwawa la Mtera, na wengine aina ya ngalala, pelage dungu, ngogo na ngobole huvuliwa wakiwa wadogo chini ya urefu wa inchi tatu, wapo hatarini kutoweka kama uvuvi haramu hautadhibitiwa..

Viongozi  na watendaji wa sekta ya uvuvi kutoka wilaya za Chamwino, Mpwawa na Iringa wamekutana mjini Iringa na kujadili namna ya kudhibiti uvuvi haramu.


Wakizungumza kwenye kikao hicho cha ujirani mwema wadau hao wa uvuvi wamependekeza kufanyika doria za pamoja kwa wilaya zote ili kuwabana wavuvi haramu wasikimbilie upande mwingine.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment