Wednesday, 5 July 2017

WAFANYAKAZI WA TAZARA FLYOVER WAGOMA

Image result for tazara flyover

WAFANYAKAZI wa kampuni ya LABA Construction Ltd ambao ni vibarua wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction company Ltd inayojenga barabara ya juu (Flyover) ya Tazara wamegoma wakishinikiza kuongezwa maslahi yao pamoja na kuitaka kampuni ya Laba kuondoka.

Wafanyakazi hao walianza mgomo kuanzia siku ya jana ambapo wanaitaka kampuni ya Laba ambayo wanadaI inafanya kazi ya udalali kuondoka kwa kuwa ndio inawanyonya kwani kampuni ya Sumitomo imekuwa ikilipa Sh 37,000 kwa fundi na kibarua Sh 25,000 lakini kampuni hiyo imekuwa ikiwalipa Sh 14,000 kwa fundi na Sh 10,000 kwa kibarua.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment