Tuesday, 4 July 2017

TFF YAFANYA MABADILIKO KAMATI YA UCHAGUZI, YUPO MJUMBE ALIYETUMWA LIPULI FC

kuuli

Baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukaa na kufikia uamuzi wa kuwaondoa katika kamati ya uchaguzi wajumbe wanne na kuweka wapya, yafuatayo ni majina ya walioondolewa na wapya.

Wajumbe walioondolewa katika kamati ya uchaguzi ni wafuatao.
1. Juma Lalika
2. Dominated Madeli
3. Jeremiah Wambura
4. Omary Hamidu

Kati ya wanne waliondolewa, Wambura yupo mjini Iringa akishughulikia sakata la uongozi wa Lipuli FC ambayo awali ilikuwa ifanye uchaguzi wake Agosti 5 kwa maelekezo ya TFF kabla Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuagiza uchaguzi wa klabu hiyo ufanyike Julai 16, mwaka huu.


Wafuatao ndiyo wajumbe wapya watakaoungana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli.

1. Mohammed Mchengela
2. Wakili Malangwe Ally
3. Wakili Kilomoni Kabamba
4. Wakili Deus Kalua


Reactions:

0 comments:

Post a Comment