Friday, 14 July 2017

SUMAYE AKERWA NA MFUMO WA DEMOKRASIA KANDAMIZI

Image result for sumaye

Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chadema, Frederick Sumaye amezungumza na vyombo vya habari hii leo na kusema kwamba nchi inakazana kujenga mfumo wa demokrasia kandamizi ambayo kwa kiasi kikubwa unarudisha nyuma maendeleo.

Amesema kuwa licha ya kukatazwa wasizungumze masuala ya kisiasa, hawatanyamaza na wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya wananchi ambao wana imani nao.

“Viongozi wa upinzani wamekuwa wakikamatwa, wanawekwa rumande, wanatishwa lengo ni kudhoofisha upinzani,” amesema Sumaye.

Amesema licha ya juhudi hizo za kuwarubuni baadhi ya viongozi wakiwamo madiwani wachache, hawatadhoofika na wataendelea kufanya Kazi.

Sumaye amesema kwamba wanataka kujenga upinzani wa kweli wenye lengo la kusaidia wananchi.


Amesema katika kulihakikisha hilo hadi kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na kijiji, mtaa utakaokuwa hauna tawi la Chadema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment