Friday, 7 July 2017

SHABANI DEDE AZIKWA MAKABURI YA KISUTU

Image result for shabani dede

Mwanamuziki mkongwe wa dansi, Shabani Dede, amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini dar es Salaam.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanamuziki pamoja na wadau wa muziki wa dansi.

Shabani Dede alipelekwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili wiki mbili zilizopita akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Alifariki jana saa mbili asubuhi akiwa anapatiwa matibabu. Mpaka mauti yanamkuta, Dede alikuwa akiitumikia bendi ya Msondo Ngoma.


Kabla ya hapo aliwahi kutumikia bendi mbali mbali kama DDC Mlimani Park, Tabora Jazz na Bima Lee.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment