Saturday, 1 July 2017

RAIS ASHAURI MUDA WA MAONESHO YA SABASABA UONGOZWE


Rais John Magufuli ameshauri kuongezwa muda kwa maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba ili kuwapa fursa wananchi wote kuhudhuria na kujionea bidhaa.

Ameyasema hayo leo (Julai 1) wakati akifungua rasmi maonyesho hayo katika viwanja vya Sabasaba na kumtaka waziri mwenye dhamana ya biashara na viwanda kulifikiria suala hilo.


“Ukiongeza muda hata siku tano au nne, hauwezi kupoteza chochote kwa sababu wananchi watakuja na watajionea , ni vizuri kama mtakubaliana kuongeza muda ili wakazi wa Dar es Salaam, wapate muda zaidi,” amesema

Reactions:

0 comments:

Post a Comment