Saturday, 8 July 2017

POLISI YAUA SITA WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI MWANZA

Image result for Kamanda wa Polisi Mwanza

Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi katika mtaa wa Fumagila Mashariki Kata ya Igoma jijini Mwanza.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo baada ya watu hao kuzingirwa katikati ya majengo mtaani hapo na kufanya mashambulizi ya kujibizana risasi kwa muda mrefu.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akaomba alitolee ufafanuzi baadaye kwa kuwa hivi sasa bado anaendelea kukusanya taarifa zaidi. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment