Wednesday, 5 July 2017

POLISI WAMUHOJI MBUNGE WA UKONGA KUHUSU TUKIO LA FUTARI ALIYOANDAA DAR

Image result for waitara mbunge

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara amehojiwa na ofisa wa polisi katika viwanja vya Bunge kwa kile alichokieleza ni kutokana na futari aliyoiandaa jimboni kwake.

Mwita amesema mahojiano hayo yanatokana na futari ambayo alimwalika Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, ambaye alitoa maneno yanayodaiwa yalionyesha kuikera Serikali.


Mahojiano kati ya Waitara na ofisa huyo yamefanyika eneo la mapokezi katika jengo la utawala la Bunge muda mchache baada ya mkutano wa saba wa Bunge kuahirishwa leo (Julai 5).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment