Friday, 21 July 2017

MWALIMU ATIWA NGUVUNI SUMBAWANGA AKIDAIWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Image result for teen pregnant in africa


MWALIMU mmoja wa shule ya sekondari Miangalua wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa kidato cha tatu.

Wakati mkuu wa shule hiyo, Gishi Milundi akikiri mwanafunzi huyo kuwa na ujauzito baada ya kufanyiwa vipimo, mzazi wa mwanafunzi huyo amesema binti yake amekiri kubeba ujauzito wa mwalimu huyo ambaye ana mahusiano naye ya kingono kwa muda mrefu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa George Kyando amesema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment