Monday, 31 July 2017

MUGABE AZUNGUMZIA AFYA YAKE, AKISEMA HAFI


RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe(93) amesema “Sifi” wakati akitupilia mbali uvumi unaohusu hali ya afya baada ya mkewe kumtaka atangaze mtu atakaye mrithi.

Mugabe amekuwa akifanya safari za matibabu za mara kwa mara nchi Singapore katika miaka ya karibuni, hali inayochochea maswali kuhusu afya yake. Safari yake ya mwisho nchini Singapore aliifanya mapema mwezi huu.

“Kumekuwa na maneno kwamba Rais anakwenda. Siendi. Kwamba Rais anakufa. Sifi,” Mugabe aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika mji wa nyumbani kwake wa Chinhoyi.


Katika mkutano huo, Mugabe anayetembea kwa shida na wakati mwingine kupoteza nguvu alitumia zaidi ya saa moja kuzungumza na wafuasi wake hao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment