Monday, 31 July 2017

MUDA WA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI UMEFIKA MWISHO

Image result for Shinzo Abe

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema yeye pamoja na Rais wa Marekani, Donald Trump wamekubaliana kuwa upo umuhimu wa kupambana na Korea ya Kaskazini katika mipango yake ya majaribio ya makombora.

Abe amewaambia waandishi wa habari kuwa anashukuru kujitolea kwa Rais Trump katika suala la Korea ya Kaskazini. Mapema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema muda wa mazungumzo umemalizika.

Haley amesema hakuna sababu ya kuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) iwapo hakutakuwa na matokeo yatakayoipa mbinyo Korea Kaskazini, na kuongeza kuwa China ni lazima iamue kama itachukua hatua mahususi dhidi ya Korea Kaskazini.


Hatua hii imekuja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lingine la makombora yake siku ya Ijumaa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment