Friday, 7 July 2017

MKUU WA WILAYA YA MBULU AKAMATA MAKINIKIA YA DHAHABU

Mkuu wa wilaya  ya mbulu Chelestino Mofuga amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika machimbo ya dhahabu Haydon na kukamata lori la tani kumi likitorosha mchanga wenye dhahabu kwenda nje ya Mbulu.

Mchango huo uliokamatwa Julai 5, mwaka huu ulidaiwa kupelekwa Singida mjini kwa lengo la kuchenjua dhahabu. 

Lori hilo lenye namba T 662 AWT Mali ya Mohamad Ali,  mkanzi wa Arusha linadaiwa kusomba trip 6 kabla ya kukamatwa. 

Mkuu wa wilaya ameagiza tajiri na dreva kushikiliwa katika kituo cha Haydon hadi uchunguzi utakapokamilika na hatua zitakazochukuliwa.


Pia amesitisha uchimbaji wa dhahabu katika eneo hilo hadi mwekezaji atakapo kamilisha mikataba na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment