Saturday, 8 July 2017

MBUNGE ALIVYOKUTANA NA WANANCHI WENYE KERO YA MAJI JIMBONI KWAKE


Wanakijiji wa kijiji cha  Magorofani Kata ya Igulwa Wilayani Bukombe Mkoani Geita ,wamelazimika kufunga barabara kwa kutumia Ndoo za kuchotea maji wakati  wa ziara ya Mbunge wa Jimbo Hilo, Dotto Biteko wakidai kero ya ukosefu wa maji kijijini kwao imekuwa sugu.

Wakizungumza katika tukio hilo, wananchi wa kijiji hicho wamesema wana shida ya maji ya muda mrefu na kwamba kisima kilichochimbwa kijijini hapo hakitoi maji kwa muda mrefu sasa.

Akikiri kuwepo kwa tatizo hilo katika kata yake, Diwani wa Kata Hiyo Richard Mabenga amesema kata hiyo yenye watu zaidi ya 22,000 ina visima vitatu tu vya maji vinavyofanya kazi.

Mhandisi wa Maji  wa wilaya hiyo aliwatoa hofu wananchi hao akisema serikali kwa kupitia bajeti yake ya 2017/2018 itajenga mtandao wa maji safi na salama utakaotoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo.

Akithibitisha mpango huo, Mbunge wa jimbo hilo alisema kuna miradi kumi ya maji itakayotekelezwa mwaka huu wa fedha na kati yake mradi mmoja umeelekezwa katika kata hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment