Thursday, 13 July 2017

MAVUNDE AZINDUA MPANGO WA URASIMISHAJI UJUZI KWA VIJANA KIGOMA

vun2

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde amezindua mpango wa Urasimishaji wa Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo kwa vijana wa Kanda ya Magharibi Mkoani Kigoma na kuwataka vijana kujitokeza kuchangamkia fursa za Mafunzo zinazotolewa na Serikali ili waweze kushiriki katika kujenga Uchumi imara kupitia Mapinduzi ya Viwanda.

Mavunde amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kugharamia mafunzo kwa Vijana elfu tatu Mia tisa 3,900 katika maeneo mbalimbali nchini hatua ambayo itawasadia kuwajengea uwezo vijana  kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Taifa kupitia Mapinduzi ya Viwanda ambapo baada ya mafunzo Serikali itawasaidia vijana kuanza kujiajiri kupitia viwanda vikubwa na vidogovidogo katika maeneo yao.

Akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa Mpango huu, Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini, Zitto Zuberi Kabwe amempongeza Naibu Waziri Mavunde pamoja na Serikali kwa kuzindua Mpango huo akisema utakasaidia vijana wa vyama vyote vya siasa, pamoja na Dini zote pasipo ubaguzi.

Zitto amesema katika uchumi wa Sasa wa Dunia nguzo pekee kwa vijana kufanikiwa baada ya Kupewa Mafunzo ni kujiunga katika vikundi vya umoja ili waweze kufikiwa kwa haraka na Serikali katika kupatiwa Mikopo na fedha zinazotengwa kwa ajili ya makundi ya vijana,na wanawake itakayowasaidia kujiajiri wenyewe.

Mpango huu unafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali na unatekelezwa kwa pamoja na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA,  Leah Lukindo amewahakikishia vijana kuwa watatumia mtandao wa vyuo vya VETA kuwafikia vijana ambao ndio walengwa wakuu wa mpango huo katika maeneo mbalimbali nchini.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment