Wednesday, 5 July 2017

MAVUNDE AAHIDI MAKUBWA KWA WAJASIRIAMALI WA DODOMAMBUNGE wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde amesema suala la kuwainua na kuwapatia elimu ya  ujasiriamali wananchi kwa azma ya kuendesha biashara zao kitaalam na kwa mpangilio utakaokuza vipato vyao kiuchumi ni mkakati endelevu na ni wa kufa na kupona.

Mavunde ambaye pi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi, Ajira na wenye Ulemavu aliyasema hayo jana wakati akifungua kongamano la Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mjasiriamali Kwanza.

Katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Cavillam mjini humo zaidi ya washiriki 2000 wamepatiwa mafunzo ya kutengeneza bidhaa,  kuchota  elimu ya ujasiriamali kwa siku nne na baadaye kuunda na kusajili vikundi vya ujasiriamali.

Baada ya usajili huo, ofisi   ya Mbunge wa Dodoma Mjini imeahidi kuvitafutia fursa  na kuvisimamia.

Alisema kimantiki na kimkakati vikundi hivyo vitapatiwa mbinu za kitaaluma na fursa za kuweza kujipatia  mikopo na mitaji ya kufanya shughuli zao, baada ya kujengewa uwezo na kupatiwa  elimu kuhusu mafunzo ya ujasiriamali na wajasiriamalu hao .

“Tutaanza kugawa kwa vikundi zikiwemo  mashine za kutengeneza chaki,mashine ya kutotoleshea mayai (Incubators), za  kutengeneza matofali za kunyonyoa manyoya ya kuku (chicken pluckers) za kushonea, zikiwemo na za kukamua juice” alisema Mavunde. 

Aidha alisema pia zitatolewa mashine za kukamlia miwa na za  kutengeneza popcorn na zile za kuchapisha yaani (heat press) ambapo jumla  gharama za mashine zote ni shiling milioni 52.

Hata hivyo mbunge huyo alisisitiza kuwa kupitia mpango kazi wa jimbo la Dodoma Mjini  wajasiriamali hao  watapatiwa fursa za kukuza vipato vyao kiuchumi na kwa mtu mmoja mmoja na hivyo kujijenga vyema kimaisha baada ya kuchangamkia fursa za  uwepo wao katika Makao Makuu ya Serikali Dodoma.

Mavunde ambaye jimboni mwake anafahamika kwa jina la "De populo Servorum" yaani Mtumishi wa watu,  aliahidi atakuwa  bega kwa bega na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa  kwa lengo la kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM  ya Mwaka 2015/2020 pia atashirikiana na mashirika hiari ya kijamii, NGOS na taasisi zinazofundisha masomo ya biashara , utoaji wa elimu na mbinu za kukuza ujasiriamali na watu kujitegemea.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment