Wednesday, 5 July 2017

MAJALIWA ASEMA HALI YA CHAKULA HAIRIDHISHI

Image result for kassim majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hali ya chakula nchini kwa sasa hairidhishi. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Julai 5) alipohitimisha shughuli za mkutano wa saba wa Bunge la 11 mjini Dodoma.

Akizungumzia hali ya chakula nchini, Waziri Mkuu amesema bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula.

“Hali ya chakula si ya kuridhisha sana, bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula,” amesema.

Majaliwa amesema hata hivyo, kuna maeneo yaliyopata mvua nyingi na chakula cha kutosha.


“Hii ni kutokana na mazao ya chakula kuanza kukomaa katika maeneo hayo. Pia, baadhi ya wakulima kuanza kuvuna mazao yao,” amesema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment