Thursday, 13 July 2017

LOWASSA ATAKIWA KURIPOTI POLISI ALHAMISI IJAYO

Image result for LOWASA POLISI

WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa ametakiwa kurudi tena Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya mahojiano siku ya Alhamisi ijayo, Julai 20 ikiwa ni nusu saa tu tangu awasili katika Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya mahojiano na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa alifika Makao Makuu ya Polisi saa 3:05 katika msafara wa magari matatu akiwa ameambatana na Wakili wake, Peter Kibatala huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na waandishi wa habari kutimuliwa kama ilivyokuwa awamu mbili zilizopita.


Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema kufika katika ofisi ya DCI kuhojiwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi. Maneno hayo anadaiwa kuyatoa Juni 23, mwaka huu katika futari iliyokuwa imeandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment