Monday, 24 July 2017

LIPUMBA ACHARUKA, ATANGAZA KUWAVUA UANACHAMA WABUNGE NANE WA CUF

Image result for Lipumba

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Profesa Lipumba limewavua uanachama wabunge nane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam kwa makosa kama hayo.

Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.

Amesema wabunge hao nane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na CHADEMA kumwondoa yeye madarakani


Reactions:

0 comments:

Post a Comment