Saturday, 1 July 2017

LIONEL MESSI AFUNGA NDOA YA KIFAHARI


DDoEkOmW0AAeg6r

Nyota wa Kandanda Duniani, Lionel Messi amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa tangu utotoni katika Mji wake wa kuzaliwa nchini Argentina.

Mchezaji huyo wa Barcelona amerejea katika Jiji la Rosario kufunga ndoa na Antonella Roccuzzo, ambaye walikutana kabla ya yeye kuhamia Uhispania akiwa na miaka 13.


Harusi hiyo imehudhuriwa na mastaa kadhaa wakiwemo wacheza soka wa zamani katika Klabu ya Barcelona kama Samuel Etoo, Carlos Puyol, Cesc Fabregas, Xavi na wengine.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment