Saturday, 8 July 2017

KINYANG'ANYIRO CHA KUMPATA MEYA MPYA DODOMA CHAANZA

Image result for MADIWANI WA DODOMA

KINYANG’ANYIRO cha kumpata Meya mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, kimeanza kwa kishindo.

Kimeanza baada ya Mkurugenzi wa Manispaa, Godwin Kunambi (pichani) kuviandikia barua juzi vyama vya siasa vyenye madiwani na kuvitaka kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo ya juu katika baraza la madiwani.

Hatua hiyo imekuja baada ya miezi mitatu kupita tangu madiwani wa Manispaa hiyo Aprili 4, mwaka huu, kumwondoa Meya wao, Jafari Mwanyemba kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha, matumizi mabaya ya ofi si na utendaji usioridhisha.


Baada ya Mwanyemba kuondolewa na kubaki kuwa diwani wa Kata ya Viwandani, Manispaa hiyo imekuwa ikiongozwa na Naibu Meya, Jumanne Ngede ambaye ni Diwani wa Chamwino.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment