Thursday, 6 July 2017

KESI YA YERICKO NYERERE KUANZA AGOSTI 7

Image result for yeriko nyerere

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itaanza kuzisikiliza kesi za uchochezi zinazomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere Agosti 7 mwaka huu.

Kesi hizo zilipaswa kuanza kusikilizwa leo (Alhamisi, Julai 6) kwa mahakimu wawili tofauti, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage lakini zimeahirishwa kwa pendekezo la Hakimu.


Yericko anayekabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kwenye mtandao wa facebook, anatetewa na mawakili, Tundu Lissu na Peter Kibatala. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment