Thursday, 6 July 2017

HAKIMU AJITOA KESI YA LEMA AKIDAIWA KUWA RAFIKI NA MKEWE

Image result for lema godbless

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia Kisinda aliyekuwa anasikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema dhidi ya Rais John Magufuli amejitoa baada ya kuwekewa pingamizi na Jamhuri kuwa ana urafiki na mke wa Lema, Neema Lema.


Hakimu huyo ni wa pili kujitoa katika kesi hiyo, kwani Mei 29, Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha pia alijitoa kwa maelezo kuwa hawezi kusikiliza kesi zote nne zinazomkabili Lema hivyo kuwaeleza mahakimu wengine watapangiwa kesi hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment