Tuesday, 4 July 2017

FIFA WAFUTA MPANGO WA KULETA WAJUMBE WAKE TFF

Image result for Wallace Karia

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limefuta mpango wake wa kutuma wawakilishi wake nchini  kwa ajili ya kufuatilia mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Taarifa hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa TFF anayekaimu nafasi ya Rais wa TFF, Wallace Karia aliyesema FIFA wamefikia uamuzi huo baada ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi wa TFF, pamoja na kupokea taarifa za maandishi.

Karia amesema katika mazungumzo hayo amewaeleza kila kitu kinachoendelea nchini, na kwamba leo Jumanne Kamati ya Utendaji inakutana.

“FIFA hawatakuja tena, tuliongea nao tukawaeleza kinachoendelea, walitupigia wakitaka kujua kama kulikuwa na muingilio wa serikali katika mchakato, au kama kuna pesa za FIFA zilizotumika vibaya, tukawaambia siyo kweli na kuwaeleza kilichotokea kwahiyo hawatakuja,” amesema Karia.

Kuhusu kikao cha leo cha kamati ya utendaji, Karia amewataka wadau wa soka nchini wakiwemo wagombea kuwa watulivu na kuiamini kamati hiyo kwani itakuja na uamuzi mzuri na wenye afya kwa mpira wa Tanzania.

Kikubwa kitakachojadiliwa katika kikao hicho ni hatma ya Kamati ya Uchaguzi ambayo wajumbe wake wameshindwa kuelewana na huenda ikapanguliwa ili kuruhusu uchaguzi uendelee.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment