Monday, 10 July 2017

CHADEMA YAJA NA OPARESHENI ONDOA MSALITI KUMSAIDIA MAALIM SEIF

Image result for kubenea

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).

Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.

Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa kujua kiini cha mgogoro huo.

“Sisi kama Chadema tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.


Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba

Reactions:

0 comments:

Post a Comment