Sunday, 9 July 2017

CCM ARUSHA YATOA ONYO KWA WAGOMBEA

Image result for ccm arusha

Katibu wa CCM wilaya ya Arusha mjini, Ramadhani Dallo amesema atawachukulia sheria wanachama wanaogombea nafasi mbalimbali ambao watagundulika kukiuka kanuni na sheria za uchaguzi.

Dallo ameyasema hayo leo wakati akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ngazi ya wilaya. Kanuni hizo ni pamoja na kutofanya kampeni, kutangaza nia au kujinadi kwa aina yoyote.

Zoezi la uchukuaji na urudishwaji fomu lilianza Julai 2 na litafungwa Julai 10.


“Katika kipindi hiki cha uchukuaji fomu na urudishwaji, wanachama pamoja na wagombea hao wanapaswa kufuata sheria na kanuni zote za uchaguzi zilizowekwa na yeyote atakayekiuka atachukuliwa sheria kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.”amesema 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment