Monday, 10 July 2017

BAADA YA KUSOTA RUMANDE KWA SIKU SITA, MDEE APATA DHAMANA

Image result for halima mdee

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa siku sita.

Mdee ameachiwa leo Julai 10, kwa dhamana ya Sh10 milioni na wadhamini wawili, baada ya kusomewa shitaka la kutumia lugha chafu na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Mbunge huyo, alikamatwa Julai 4 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliyeamuru awekwe mahabusu kwa saa 48.

Hapi alidai, Mdee amemkashifu Rais na ndicho chanzo cha kutupwa rumande kwa saa hizo.

Wakili wa Serikali Nassoro Katuga amedai kuwa Mdee akiwa Makao Makuu ya ofisi ya Chadema alitoa lugha chafu dhidi ya Rais.


Upelelezi bado haujakamilika lakini Mdee amepata dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao wao pamoja na yeye wamesaini bondi ya Sh 10milioni.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment